Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 25:4-16 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Watoto wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.

5. Abrahamu alimrithisha Isaka mali yake yote.

6. Lakini watoto wa kiume wa masuria wake akawapa zawadi, na wakati alipokuwa bado hai, aliwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka mwanawe.

7. Abrahamu aliishi miaka 175.

8. Alifariki baada ya kuishi maisha marefu na ya fanaka, akajiunga na wazee wake waliomtangulia.

9. Isaka na Ishmaeli, wanawe Abrahamu, wakamzika baba yao katika pango la Makpela, mashariki ya Mamre kwenye shamba lililokuwa la Efroni, mwana wa Sohari, Mhiti.

10. Abrahamu alikuwa amenunua shamba hilo kwa Wahiti. Huko ndiko alikozikwa Abrahamu na mkewe Sara.

11. Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu alimbariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akawa anaishi karibu na kisima cha Beer-lahai-roi.

12. Hawa ndio wazawa wa Ishmaeli mwanawe Abrahamu ambaye Hagari Mmisri, aliyekuwa mjakazi wa Sara, alimzalia Abrahamu.

13. Hii ni orodha yao kufuatana na kuzaliwa kwao: Nebayothi, mzaliwa wa kwanza, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,

14. Mishma, Duma, Masa,

15. Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema.

16. Hao ndio watoto wa kiume wa Ishmaeli, waliokuwa asili ya makabila kumi na mawili; makazi na vijiji vyao vilijulikana kwa majina yao.

Kusoma sura kamili Mwanzo 25