Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 24:20-30 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Basi, akafanya haraka, akawamiminia ngamia maji ya mtungi wake katika hori, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na kuwanywesha ngamia wake wote.

21. Yule mtu akawa anamtazama kwa makini bila kusema lolote, apate kufahamu kama Mwenyezi-Mungu ameifanikisha safari yake au sivyo.

22. Ngamia walipotosheka kunywa maji, yule mtu akampa huyo msichana pete ya dhahabu yenye uzito upatao gramu sita, na bangili mbili za dhahabu za gramu kumi kila moja.

23. Akamwuliza, “Niambie tafadhali: Wewe ni binti nani? Je, kuna nafasi ya kulala nyumbani kwenu?”

24. Rebeka akajibu, “Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Milka, mkewe Nahori.

25. Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha na mahali pa kulala wageni.”

26. Ndipo yule mtu akainamisha kichwa chake, akamwabudu Mwenyezi-Mungu

27. akisema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hajasahau fadhili zake na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mwenyezi-Mungu ameniongoza mimi mwenyewe moja kwa moja hadi kwa jamaa ya bwana wangu!”

28. Kisha yule msichana akakimbia kwenda kuwapa habari jamaa za mama yake.

29. Rebeka alikuwa na kaka yake aitwaye Labani. Labani akatoka mbio kukutana na yule mtu kisimani.

30. Labani alikuwa ameiona ile pete na bangili mikononi mwa dada yake, na kusikia mambo Rebeka aliyoambiwa na huyo mtu. Labani alimkuta yule mtu amesimama karibu na ngamia wake kando ya kisima.

Kusoma sura kamili Mwanzo 24