Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 23:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sara aliishi miaka 127. Hiyo ndiyo iliyokuwa miaka ya maisha yake Sara.

2. Alifia huko Kiriath-arba, yaani Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abrahamu akaomboleza na kumfanyia matanga Sara mkewe.

3. Abrahamu akaiacha maiti ya mkewe, akatoka kwenda kuzungumza na Wahiti, akawaambia,

4. “Mimi ninaishi kama mgeni miongoni mwenu. Nipatieni sehemu ya ardhi ya kaburi, ili nipate kumzika marehemu mke wangu.”

Kusoma sura kamili Mwanzo 23