Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 2:18-25 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Si vizuri huyu mwanamume kuwa peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

19. Basi, kutoka katika udongo, Mwenyezi-Mungu akaumba kila mnyama wa porini na kila ndege wa angani, halafu akamletea huyo mwanamume aone atawapa majina gani; na majina aliyowapa viumbe hao, yakawa ndio majina yao.

20. Basi, huyo mwanamume akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, wanyama wa porini na ndege wote wa angani. Lakini hakupatikana msaidizi yeyote wa kumfaa.

21. Basi, Mwenyezi-Mungu akamletea huyo mwanamume usingizi mzito, na alipokuwa usingizini, akatwaa ubavu wake mmoja na kupafunika mahali pale kwa nyama.

22. Na huo ubavu Mwenyezi-Mungu alioutoa kwa yule mwanamume akaufanya kuwa mwanamke, akamleta kwa huyo mwanamume.

23. Ndipo huyo mwanamume akasema,“Naam! Huyu ni mfupa kutoka mifupa yangu,na nyama kutoka nyama yangu.Huyu ataitwa ‘Mwanamke’,kwa sababu ametolewa katika mwanamume.”

24. Ndiyo maana mwanamume humwacha baba yake na mama yake, akaambatana na mkewe, nao wawili huwa mwili mmoja.

25. Huyo mwanamume na mkewe wote walikuwa uchi, lakini hawakuona haya.

Kusoma sura kamili Mwanzo 2