Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 17:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wakati Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi-Mungu alimtokea, akamwambia, “Mimi ni Mungu mwenye nguvu. Fuata mwongozo wangu na kuishi bila lawama.

2. Nami nitafanya agano nawe na kuwazidisha wazawa wako.”

3. Hapo Abramu akasujudu. Naye Mungu akamwambia,

4. “Ninafanya agano hili nawe: Utakuwa baba wa mataifa mengi.

5. Tangu sasa, hutaitwa tena Abramu, bali utaitwa Abrahamu, maana nimekufanya kuwa baba wa mataifa mengi.

6. Nitakufanya uwe na wazawa wengi sana; kwako nitazusha mataifa mengi na wafalme.

7. Nitalithibitisha agano langu nawe, wazawa wako na vizazi vyao vyote milele; tena nitakuwa Mungu wako na Mungu wa wazawa wako milele.

8. Nitakupa wewe na wazawa wako nchi hii ambamo unaishi kama mgeni; yaani nchi yote ya Kanaani iwe mali yenu milele; nami nitakuwa Mungu wao.”

9. Kisha Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, wewe utalishika agano langu, wewe binafsi, wazawa wako na vizazi vyao vyote.

Kusoma sura kamili Mwanzo 17