Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 11:20-32 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Reu alipokuwa na umri wa miaka 32, alimzaa Serugi.

21. Baada ya kumzaa Serugi, Reu aliishi miaka 207 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

22. Serugi alipokuwa na umri wa miaka 30, alimzaa Nahori.

23. Baada ya kumzaa Nahori, Serugi aliishi miaka 200 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

24. Nahori alipokuwa na umri wa miaka 29, alimzaa Tera.

25. Baada ya kumzaa Tera, Nahori aliishi miaka 119, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

26. Tera alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Abramu na Nahori na Harani.

27. Wafuatao ni wazawa wa Tera, baba yao Abramu, Nahori na Harani. Harani alikuwa baba yake Loti.

28. Huyo Harani alifariki wakati Tera baba yake alikuwa anaishi huko Uri alikokuwa amezaliwa.

29. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai. Mke wa Nahori aliitwa Milka, binti Harani ambaye pia alikuwa baba yake Iska.

30. Sarai hakuwa na mtoto kwa sababu alikuwa tasa.

31. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mjukuu wake aliyekuwa mwanawe Harani, na Sarai mkewe Abramu, wakaondoka wote pamoja toka Uri, mji wa Wakaldayo, wakaenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakakaa.

32. Tera alifariki huko Harani akiwa na umri wa miaka 205.

Kusoma sura kamili Mwanzo 11