Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 1:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia.

2. Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.

3. Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa.

4. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza,

5. mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.

6. Mungu akasema, “Anga liwe katikati ya maji, liyatenge maji sehemu mbili.”

7. Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.

8. Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili.

9. Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, nchi kavu itokee.” Ikawa hivyo.

10. Mungu akapaita mahali pakavu “Nchi” na kusanyiko la maji akaliita “Bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.

Kusoma sura kamili Mwanzo 1