Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 7:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Lakini mimi namtumainia Mwenyezi-Mungu,namtazamia Mungu mwenye kuniokoa;Mungu wangu atanisikiliza.

8. Usifurahie maafa yangu ewe adui yangu!Nikianguka, nitainuka tena;Nikiwa gizani, Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu.

9. Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu,sina budi kuvumilia ghadhabu yake,mpaka atakapotetea kisa changuna kunijalia haki yangu.Atanileta nje kwenye mwanga,nami nitaona akithibitisha haki.

10. Hapo adui yangu ataona hayonaye atajaa aibu;maana aliniambia: “Wapi basi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako?”Mimi mwenyewe nitamwona adui akianguka;atakanyagwakanyagwa chini kama tope la njiani.

11. Siku yaja ambapo kuta za mji wenu zitajengwa upya.Siku hiyo mipaka ya nchi yenu itapanuliwa.

12. Siku hiyo ndugu zenu watawarudia,kutoka Ashuru na vijiji vya Misri,kutoka nchi ya Misri na eneo la Eufrate;kutoka sehemu za maji na sehemu za milima.

13. Lakini nchi yote nyingine itakuwa jangwa,kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.

Kusoma sura kamili Mika 7