Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 7:3-15 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Wote ni mabingwa wa kutenda maovu;viongozi na mahakimu hutaka rushwa.Wakubwa huonesha wazi nia zao mbaya,na kufanya hila kuzitekeleza.

4. Mwema zaidi kati yao hutaabisha kama mbigili,aliye mnyofu zaidi ni kama ua wa miiba.Siku iliyongojewa ya adhabu yao imefika.Na sasa mahangaiko yamewakumba.

5. Usimwamini mwenzako,wala usimtumainie rafiki yako.Chunga unachosema kwa mdomo wako,hata na mke wako wewe mwenyewe.

6. Maana, mtoto wa kiume anamdharau baba yake;mtoto wa kike anashindana na mama yake,mke wa mwana anapingana na mama mkwe wake.Maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.

7. Lakini mimi namtumainia Mwenyezi-Mungu,namtazamia Mungu mwenye kuniokoa;Mungu wangu atanisikiliza.

8. Usifurahie maafa yangu ewe adui yangu!Nikianguka, nitainuka tena;Nikiwa gizani, Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu.

9. Kwa vile nimemkosea Mwenyezi-Mungu,sina budi kuvumilia ghadhabu yake,mpaka atakapotetea kisa changuna kunijalia haki yangu.Atanileta nje kwenye mwanga,nami nitaona akithibitisha haki.

10. Hapo adui yangu ataona hayonaye atajaa aibu;maana aliniambia: “Wapi basi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako?”Mimi mwenyewe nitamwona adui akianguka;atakanyagwakanyagwa chini kama tope la njiani.

11. Siku yaja ambapo kuta za mji wenu zitajengwa upya.Siku hiyo mipaka ya nchi yenu itapanuliwa.

12. Siku hiyo ndugu zenu watawarudia,kutoka Ashuru na vijiji vya Misri,kutoka nchi ya Misri na eneo la Eufrate;kutoka sehemu za maji na sehemu za milima.

13. Lakini nchi yote nyingine itakuwa jangwa,kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.

14. Ee Mungu, uwachunge watu wako kwa fimbo yako,uwachunge hao walio kundi lako mwenyeweambao wanaishi peke yao katika msituwamezungukwa na ardhi yenye rutuba.Uwachunge kama ulivyofanya pale awalikatika malisho ya Bashani na Gileadi.

15. Kama wakati ulipotutoa nchini Misri,utuoneshe tena maajabu yako.

Kusoma sura kamili Mika 7