Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 7:10-20 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Hapo adui yangu ataona hayonaye atajaa aibu;maana aliniambia: “Wapi basi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako?”Mimi mwenyewe nitamwona adui akianguka;atakanyagwakanyagwa chini kama tope la njiani.

11. Siku yaja ambapo kuta za mji wenu zitajengwa upya.Siku hiyo mipaka ya nchi yenu itapanuliwa.

12. Siku hiyo ndugu zenu watawarudia,kutoka Ashuru na vijiji vya Misri,kutoka nchi ya Misri na eneo la Eufrate;kutoka sehemu za maji na sehemu za milima.

13. Lakini nchi yote nyingine itakuwa jangwa,kwa sababu ya uovu wa wakazi wake.

14. Ee Mungu, uwachunge watu wako kwa fimbo yako,uwachunge hao walio kundi lako mwenyeweambao wanaishi peke yao katika msituwamezungukwa na ardhi yenye rutuba.Uwachunge kama ulivyofanya pale awalikatika malisho ya Bashani na Gileadi.

15. Kama wakati ulipotutoa nchini Misri,utuoneshe tena maajabu yako.

16. Nao watu wa mataifa watakapoona hayo,watajaa fedheha hata kama wana nguvu.Watashikwa na bumbuazi na kukosa cha kusemana kuwa kama viziwi.

17. Watatambaa mavumbini kama nyoka;naam, kama viumbe watambaao.Watatoka katika ngome zaohuku wanatetemeka na kujaa hofu.Watakugeukia wewe Mungu wetu kwa hofu,wataogopa kwa sababu yako.

18. Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?Wewe wasamehe dhambi za watu wako waliobaki,wala huyaangalii makosa yao.Hasira yako haidumu milele,ila wapendelea zaidi kutuonesha fadhili zako.

19. Utatuhurumia tena, ee Mwenyezi-Mungu;utafutilia mbali dhambi zetu,utazitupa zote katika vilindi vya bahari.

20. Utaonesha uaminifu wako na rehema zakokwa wazawa wa Abrahamu na wa Yakobo,kama ulivyowaahidi wazee wetu tangu zamani.

Kusoma sura kamili Mika 7