Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 4:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Hao walemavu ndio watakaobaki hai;hao waliochukuliwa uhamishoni watakuwa taifa lenye nguvu.Nami Mwenyezi-Mungu nitawatawala mlimani Siyoni,tangu wakati huo na hata milele.”

8. Nawe kilima cha Yerusalemu,wewe ngome ya Siyoni,ambamo Mungu anafanya ulinzi juu ya watu wake,kama mchungaji juu ya kondoo wake;wewe utakuwa tena mji maarufu kama hapo awali,Yerusalemu utakuwa tena mji mkuu wa mfalme.

9. Sasa kwa nini mnalia kwa sauti?Je, hamna mfalme tena?Mshauri wenu ametoweka?Mnapaza sauti ya uchungu,kama mama anayejifungua!

10. Enyi watu wa Siyoni,lieni na kugaagaa kama mama anayejifungua!Maana sasa mtaondoka katika mji huumwende kukaa nyikani,mtakwenda mpaka Babuloni.Lakini huko, mtaokolewa.Huko Mwenyezi-Mungu atawakomboa makuchani mwa adui zenu.

11. Mataifa mengi yamekusanyika kuwashambulia.Yanasema: “Acheni mji wao utiwe najisi,nasi tuyaone magofu ya Siyoni!”

12. Lakini waohawafahamu mawazo ya Mwenyezi-Munguwala hawaelewi mpango wake:Kwamba amewakusanya pamoja,kama miganda mahali pa kupuria.

13. Mwenyezi-Mungu asema,“Enyi watu wa Siyoni,inukeni mkawaadhibu adui zenu!Nitawapeni nguvu kama fahalimwenye pembe za chuma na kwato za shaba.Mtawasaga watu wa mataifa mengi;mapato yao mtaniwekea wakfu mimi,mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”

Kusoma sura kamili Mika 4