Agano la Kale

Agano Jipya

Mika 4:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Utakuja wakati ambapomlima wa nyumba ya Mwenyezi-Munguutakuwa mkubwa kuliko milima yote.Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote.Watu wengi watamiminika huko,

2. mataifa mengi yataujia na kusema:“Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu,twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo,ili atufundishe njia zake,nasi tufuate nyayo zake.Maana mwongozo utatoka huko Siyoni;neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.”

3. Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa mengi,atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali.Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe,na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea.Taifa halitapigana na taifa lingine,wala hayatafanya tena mazoezi ya vita.

4. Kila mtu atakaa kwa amanichini ya mitini na mizabibu yake,bila kutishwa na mtu yeyote.Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ametamka yeye mwenyewe.

5. Mataifa mengine hufuata njia zao,kwa kuitegemea miungu yao,lakini sisi twafuata njia zetu kwa kumtegemea Mwenyezi-Mungu,Mungu wetu, milele na milele.

Kusoma sura kamili Mika 4