Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 9:3-8 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Hili ni jambo baya zaidi kati ya yote yatukiayo hapa duniani, kwamba mwisho uleule huwapata wote. Tena, wakati wote wa maisha yao, wanadamu huwa wamejaa uovu na wazimu, na kisha hufa.

4. Lakini anayeambatana na walio hai analo bado tumaini, afadhali mbwa hai kuliko simba mfu.

5. Maana, walio hai hujua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote. Hawana tuzo tena; hata kumbukumbu lao limesahauliwa kabisa.

6. Upendo wao, chuki zao na tamaa zao, vyote vimetoweka pamoja nao, na wala hawatashiriki chochote hapa duniani.

7. Nenda ukale chakula chako kwa furaha, ukanywe na divai yako kwa moyo mchangamfu, maana Mungu amekwisha ikubali kazi yako.

8. Vaa vizuri, jipake mafuta kichwani.

Kusoma sura kamili Mhubiri 9