Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 9:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)

2. maana mwisho uleule huwapata waadilifu na waovu, wema na wabaya, walio safi na walio najisi, wenye kutoa sadaka na wasiotoa sadaka. Aliye mwema ni sawa tu na mwenye dhambi, na mwenye kuapa si tofauti na asiyeapa.

3. Hili ni jambo baya zaidi kati ya yote yatukiayo hapa duniani, kwamba mwisho uleule huwapata wote. Tena, wakati wote wa maisha yao, wanadamu huwa wamejaa uovu na wazimu, na kisha hufa.

4. Lakini anayeambatana na walio hai analo bado tumaini, afadhali mbwa hai kuliko simba mfu.

5. Maana, walio hai hujua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote. Hawana tuzo tena; hata kumbukumbu lao limesahauliwa kabisa.

Kusoma sura kamili Mhubiri 9