Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 3:5-16 Biblia Habari Njema (BHN)

5. wakati wa kutupa mawe na wakati wa kuyakusanya mawe pamoja;wakati wa kukumbatia na wakati wa kuacha kukumbatia;

6. wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza;wakati wa kuhifadhi na wakati wa kutupa;

7. wakati wa kurarua na wakati wa kushona;wakati wa kukaa kimya na wakati wa kuongea;

8. wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia;wakati wa vita na wakati wa amani.

9. Mfanyakazi hufaidi nini kutokana na juhudi zake hizo?

10. Mimi nimeiona kazi ambayo binadamu amepewa na Mungu.

11. Mungu amekifanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Amempa binadamu hamu ya kujua mambo ya baadaye, lakini hajamjalia fursa ya kuelewa matendo yake Mungu tangu mwanzo mpaka mwisho.

12. Najua kwamba, kwa binadamu, liko jambo moja tu la kumfaa; kufurahi na kujifurahisha muda wote aishipo.

13. Sote inatupasa kula na kunywa na kufurahia matunda ya kazi zetu. Hayo ni majaliwa ya Mungu.

14. Najua kwamba lolote atendalo Mungu linadumu milele. Hakuna kinachoweza kuongezwa wala kupunguzwa; Mungu amefanya mambo yawe hivyo kusudi wanadamu wamche yeye.

15. Kinachotukia sasa, kilikwisha tukia; kitakachotukia baadaye kilikwisha tukia; na Mungu hukifanya kitu kilekile kitukie tena na tena.

16. Zaidi ya hayo, nimegundua duniani kwamba, mahali pa haki na uadilifu, uovu unatawala.

Kusoma sura kamili Mhubiri 3