Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 10:7-16 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Nimeona watumwa wanapanda farasi, na wakuu wanatembea kwa miguu kama watumwa.

8. Mchimba shimo hutumbukia mwenyewe,abomoaye ukuta huumwa na nyoka.

9. Mchonga mawe huumizwa nayo,mkata kuni hukabiliwa na hatari.

10. Nguvu nyingi zaidi zahitajikakwa mtumiaji shoka butu lisilonolewa,lakini kutumia hekima humfanya mtu afanikiwe.

11. Nyoka akiuma kabla hajachochewa,mchochezi hahitajiki tena.

12. Maneno ya mwenye hekima humnufaisha asemaye;lakini midomo ya mpumbavu humwangamiza.

13. Mpumbavu huanza kusema kwa maneno ya kijinga,na kumaliza kauli yake kwa wazimu mbaya.

14. Mpumbavu hububujika maneno.Binadamu hajui yatakayokuwako,wala yale yatakayotukia baada yake.

15. Mpumbavu huchoshwa na kazi yakehata asijue njia ya kurudia nyumbani.

16. Ole wako, ewe nchi, mtawala wako akiwa kijana,na viongozi wako wakifanya sherehe asubuhi.

Kusoma sura kamili Mhubiri 10