Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 10:3-13 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Hata apitapo njiani, mpumbavu hutambulikana hivyo,humjulisha kila mtu kwamba yeye ni mpumbavu.

4. Mtawala akikuwakia hasira, usijiuzulu;makosa makubwa huweza kufutwa ukiwa mnyenyekevu.

5. Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala:

6. Kwamba wapumbavu wanapewa kazi za madaraka ya juu, na matajiri wanachukua nafasi za mwisho.

7. Nimeona watumwa wanapanda farasi, na wakuu wanatembea kwa miguu kama watumwa.

8. Mchimba shimo hutumbukia mwenyewe,abomoaye ukuta huumwa na nyoka.

9. Mchonga mawe huumizwa nayo,mkata kuni hukabiliwa na hatari.

10. Nguvu nyingi zaidi zahitajikakwa mtumiaji shoka butu lisilonolewa,lakini kutumia hekima humfanya mtu afanikiwe.

11. Nyoka akiuma kabla hajachochewa,mchochezi hahitajiki tena.

12. Maneno ya mwenye hekima humnufaisha asemaye;lakini midomo ya mpumbavu humwangamiza.

13. Mpumbavu huanza kusema kwa maneno ya kijinga,na kumaliza kauli yake kwa wazimu mbaya.

Kusoma sura kamili Mhubiri 10