Agano la Kale

Agano Jipya

Mhubiri 10:13-20 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Mpumbavu huanza kusema kwa maneno ya kijinga,na kumaliza kauli yake kwa wazimu mbaya.

14. Mpumbavu hububujika maneno.Binadamu hajui yatakayokuwako,wala yale yatakayotukia baada yake.

15. Mpumbavu huchoshwa na kazi yakehata asijue njia ya kurudia nyumbani.

16. Ole wako, ewe nchi, mtawala wako akiwa kijana,na viongozi wako wakifanya sherehe asubuhi.

17. Heri yako, ewe nchi, mtawala wako akiwa mtu wa heshima,na viongozi wako wakifanya sherehe wakati wa kufaa,ili kujipatia nguvu na si kujilewesha.

18. Kutokana na uvivu wa mtu, paa hubonyea;kwa sababu ya uzembe, nyumba huvuja.

19. Chakula ni kwa ajili ya kujifurahisha,divai huchangamsha maisha;na fedha husababisha hayo yote.

20. Usimwapize mtawala hata moyoni mwako,wala usimwapize tajiri hata chumbani mwako unakolala,kwa kuwa ndege ataisikia sauti yako,au kiumbe arukaye atatangaza maneno yako.

Kusoma sura kamili Mhubiri 10