Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 7:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Amechukua bunda la fedha;hatarejea nyumbani karibuni.”

21. Alimshawishi kwa maneno mengi ya kubembeleza;kijana akashawishika kwa maneno yake matamu.

22. Hapo akamfuata huyo mwanamke moja kwa moja,kama ng'ombe aendaye machinjioni,kama paa arukiaye mtegoni.

23. Hakutambua kwamba hiyo itamgharimu maisha yake,mpaka alipojikuta amekuwa kama amechomwa mshale moyoni,amekuwa kama ndege aliyenaswa wavuni.

24. Sasa wanangu, nisikilizeni;yategeeni sikio maneno ya kinywa changu.

25. Msikubali kuongozwa na mwanamke kama huyo,wala msipitepite katika mapito yake.

26. Maana amewaangusha wanaume wengi;ni wengi mno hao aliowachinja.

27. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu,ni mahali pa kuteremkia mautini.

Kusoma sura kamili Methali 7