Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 7:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwanangu, yashike maneno yangu,zihifadhi kwako amri zangu.

2. Zifuate amri zangu nawe utaishi;yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.

3. Yafunge vidoleni mwako;yaandike moyoni mwako.

4. Iambie Hekima: “Wewe ni dada yangu”,na Busara “Wewe ni rafiki yangu”.

5. Vitakulinda mbali na mwanamke mbaya,vitakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.

6. Siku moja dirishani mwa nyumba yangu,nilichungulia nje kupitia viunzi vya dirisha,

7. nikawaona vijana wengi wajinga,na mmoja hasa aliyekuwa mpumbavu.

8. Huyo alikuwa akitembea kwenye barabara ile,karibu na kona alikoishi mwanamke fulani.Basi akashika njia iendayo nyumbani kwa mwanamke huyo.

9. Ilikuwa yapata wakati wa jioni,giza na usiku vilikuwa vimeanza kuingia.

10. Punde kijana akakutana na huyo mwanamke;amevalia kama malaya, ana mipango yake.

Kusoma sura kamili Methali 7