Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 31:8-17 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;na kutetea haki za wote wasiojiweza.

9. Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,linda haki za maskini na fukara.

10. Mke mwema kweli, apatikana wapi?Huyo ana thamani kuliko johari!

11. Mumewe humwamini kwa moyo,kwake atapata faida daima.

12. Kamwe hamtendei mumewe mabaya,bali humtendea mema maisha yake yote.

13. Hutafuta sufu na kitani,na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.

14. Yeye ni kama meli za biashara:Huleta chakula chake kutoka mbali.

15. Huamka kabla ya mapambazuko,akaitayarishia jamaa yake chakula,na kuwagawia kazi watumishi wake.

16. Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua,na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.

17. Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvuna kuiimarisha mikono yake.

Kusoma sura kamili Methali 31