Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 31:21-31 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.

22. Hujitengenezea matandiko,mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.

23. Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.

24. Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,huwauzia wafanyabiashara mishipi.

25. Nguvu na heshima ndizo sifa zake,hucheka afikiriapo wakati ujao.

26. Hufungua kinywa kunena kwa hekima,huwashauri wengine kwa wema.

27. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,kamwe hakai bure hata kidogo.

28. Watoto wake huamka na kumshukuru,mumewe huimba sifa zake.

29. Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu,lakini wewe umewashinda wote.”

30. Madaha huhadaa na uzuri haufai,bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.

31. Jasho lake lastahili kulipwa,shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.

Kusoma sura kamili Methali 31