Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 31:18-28 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Hutambua kwamba shughuli zake zina faida;hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.

19. Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe,kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.

20. Huufungua mkono wake kuwapa maskini,hunyosha mkono kuwasaidia fukara.

21. Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.

22. Hujitengenezea matandiko,mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.

23. Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.

24. Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,huwauzia wafanyabiashara mishipi.

25. Nguvu na heshima ndizo sifa zake,hucheka afikiriapo wakati ujao.

26. Hufungua kinywa kunena kwa hekima,huwashauri wengine kwa wema.

27. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,kamwe hakai bure hata kidogo.

28. Watoto wake huamka na kumshukuru,mumewe huimba sifa zake.

Kusoma sura kamili Methali 31