Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 31:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:

2. Nikuambie nini mwanangu?Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?

3. Usimalize nguvu zako kwa wanawake,usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.

4. Haifai ee Lemueli, haifai wafalme kunywa divai,wala wakuu kutamani vileo.

5. Wakinywa watasahau maagizo ya sheria,na kuwanyima haki wenye taabu.

6. Mpe kileo mtu anayekufa,wape divai wale wenye huzuni tele;

7. wanywe na kusahau umaskini wao,wasikumbuke tena taabu yao.

8. Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;na kutetea haki za wote wasiojiweza.

9. Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,linda haki za maskini na fukara.

10. Mke mwema kweli, apatikana wapi?Huyo ana thamani kuliko johari!

11. Mumewe humwamini kwa moyo,kwake atapata faida daima.

12. Kamwe hamtendei mumewe mabaya,bali humtendea mema maisha yake yote.

13. Hutafuta sufu na kitani,na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.

14. Yeye ni kama meli za biashara:Huleta chakula chake kutoka mbali.

15. Huamka kabla ya mapambazuko,akaitayarishia jamaa yake chakula,na kuwagawia kazi watumishi wake.

Kusoma sura kamili Methali 31