Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 3:16-31 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu;kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.

17. Njia zake ni za kupendeza,zote zaelekea kwenye amani.

18. Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;wana heri wote wanaoshikamana naye.

19. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,kwa akili aliziimarisha mbingu.

20. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,na mawingu yakadondosha umande.

21. Mwanangu, zingatia hekima safi na busara;usiviache vitoweke machoni pako,

22. navyo vitakuwa uhai nafsini mwako,na pambo zuri shingoni mwako.

23. Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama,wala mguu wako hautajikwaa.

24. Ukiketi hutakuwa na hofu;ukilala utapata usingizi mtamu.

25. Usiogope juu ya tishio la ghafla,wala shambulio kutoka kwa waovu,

26. Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.

27. Usimnyime mtu anayehitaji msaada,ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.

28. Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho,hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.

29. Usipange maovu dhidi ya jirani yako,anayeishi karibu nawe bila wasiwasi.

30. Usigombane na mtu bila sababuikiwa hajakudhuru kwa lolote.

31. Usimwonee wivu mtu mkatili,wala usiige mwenendo wake.

Kusoma sura kamili Methali 3