Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 3:15-26 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Hekima ina thamani kuliko johari,hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.

16. Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu;kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.

17. Njia zake ni za kupendeza,zote zaelekea kwenye amani.

18. Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;wana heri wote wanaoshikamana naye.

19. Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,kwa akili aliziimarisha mbingu.

20. Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,na mawingu yakadondosha umande.

21. Mwanangu, zingatia hekima safi na busara;usiviache vitoweke machoni pako,

22. navyo vitakuwa uhai nafsini mwako,na pambo zuri shingoni mwako.

23. Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama,wala mguu wako hautajikwaa.

24. Ukiketi hutakuwa na hofu;ukilala utapata usingizi mtamu.

25. Usiogope juu ya tishio la ghafla,wala shambulio kutoka kwa waovu,

26. Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.

Kusoma sura kamili Methali 3