Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 29:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Anayeonywa mara nyingi akawa mkaidi,ataangamia ghafla asipone tena.

2. Waadilifu wakitawala watu hufurahi,lakini waovu wakitawala watu hulalamika.

3. Apendaye hekima humfurahisha baba yake;lakini aandamanaye na malaya hufuja mali yake.

4. Mfalme akitumia haki huipatia nchi uthabiti,lakini akipenda hongo taifa huangamia.

5. Mwenye kumbembeleza jirani yake,anatega mtego wa kujinasa mwenyewe.

6. Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake,lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi.

7. Mwadilifu anajua haki za maskini,lakini mtu mwovu hajui mambo hayo.

8. Wenye dharau huutia vurugu mji mzima,lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu.

9. Mwenye hekima akibishana na mpumbavu,mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia.

10. Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia,lakini watu wema huyalinda maisha yake.

Kusoma sura kamili Methali 29