25. Mchoyo huchochea ugomvi,lakini anayemtegemea Mwenyezi-Mungu atafanikiwa.
26. Anayetegemea akili yake mwenyewe ni mpumbavu;lakini anayeishi kwa hekima atakuwa salama.
27. Aliye mkarimu kwa maskini hatatindikiwa kitu,lakini anayekataa kuwaangalia atalaaniwa kwa wingi.
28. Waovu wakitawala watu hujificha,lakini wakiangamia, waadilifu huongezeka.