Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 28:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu,lakini waadilifu ni hodari kama simba.

2. Taifa la fujo huzusha viongozi wengi,lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano

3. Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini,amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea.

4. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu,lakini wanaoishika sheria hupingana nao.

5. Waovu hawajui maana ya haki,lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.

6. Afadhali maskini aishiye kwa unyofu,kuliko tajiri aishiye kwa upotovu.

7. Mtoto ashikaye sheria ni mwenye hekima,lakini rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

8. Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faidaanamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini.

Kusoma sura kamili Methali 28