Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 26:1-20 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Heshima apewayo mpumbavu haimfai;ni kama theluji ya kiangazi,au mvua ya wakati wa mavuno.

2. Kama shomoro au mbayuwayu wasiotua,kadhalika laana asiyostahili mtu haimtui.

3. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.

4. Usimjibu mpumbavu kipumbavu,usije ukafanana naye.

5. Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake,asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi.

6. Kumtuma mpumbavu ujumbe,ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida.

7. Methali mdomoni mwa mpumbavu,ni kama miguu ya kiwete inayoninginia.

8. Kumpa mpumbavu heshima,ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo.

9. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali,ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi.

10. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi,ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu.

11. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake,ni kama mbwa anayekula matapishi yake.

12. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima?Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.

13. Mvivu husema: “Huko nje kuna simba;siwezi kwenda huko.”

14. Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake,ndivyo mvivu juu ya kitanda chake.

15. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula,lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni.

16. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekimakuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

17. Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu,ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita.

18. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge,au mishale ya kifo,

19. ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani,kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!”

20. Bila kuni, moto huzimika;bila mchochezi, ugomvi humalizika.

Kusoma sura kamili Methali 26