Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 24:14-24 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako;ukiipata utakuwa na matazamio mema,wala tumaini lako halitakuwa la bure.

15. Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema,wala usijaribu kuiharibu nyumba yake,

16. maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka,lakini mtu mwovu huangamizwa na janga.

17. Usishangilie kuanguka kwa adui yako;usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake,

18. maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa;huenda akaacha kumwadhibu.

19. Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya,wala usiwaonee wivu watu waovu,

20. maana mwovu hatakuwa na mema baadaye;taa ya uhai wake itazimwa.

21. Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme,wala usishirikiane na wale wasio na msimamo,

22. maana maangamizi yao huwapata ghafla.Hakuna ajuaye maafa watakayozusha.

23. Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima:Kupendelea watu katika hukumu si vizuri.

24. Anayemwachilia mtu mwenye hatia,hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa.

Kusoma sura kamili Methali 24