Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 24:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Usiwaonee wivu watu waovu,wala usitamani kuwa pamoja nao,

2. maana fikira zao zote ni juu ya ukatili,hamna jema lolote litokalo midomoni mwao.

3. Nyumba hujengwa kwa hekima,na kuimarishwa kwa busara.

4. Kwa maarifa vyumba vyake hujazwavitu vya thamani na vya kupendeza.

5. Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu,naam, maarifa ni bora kuliko nguvu.

6. Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita,na kwa washauri wengi ushindi hupatikana.

7. Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa;penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo.

8. Afikiriaye kutenda maovu daimaataitwa mtu mwenye fitina.

9. Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi;mwenye dharau huchukiwa na kila mtu.

10. Ukifa moyo wakati wa shida,basi wewe ni dhaifu kweli.

11. Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure;usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia.

12. Usiseme baadaye: “Hatukujua!”Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona;yeye atakulipa kulingana na matendo yako!

13. Mwanangu, ule asali maana ni nzuri;sega la asali ni tamu mdomoni.

Kusoma sura kamili Methali 24