Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 21:22-31 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Mwenye hekima aweza kuteka mji wa wenye nguvu,na kuziporomosha ngome wanazozitegemea.

23. Achungaye mdomo wake na ulimi wake,hujiepusha na matatizo.

24. Mwenye majivuno na kiburi jina lake ni “Madharau;”matendo yake yamejaa majivuno ya ufidhuli wake.

25. Mvivu hufa kwa kutotimizwa tamaa zake,maana mikono yake milegevu haitaki kufanya kazi.

26. Mchana kutwa mwovu hutamani kupata kitu,lakini mwadilifu hutoa, tena kwa ukarimu.

27. Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza,huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya.

28. Shahidi mwongo ataangamia,lakini msikivu hawezi kunyamazishwa.

29. Mtu mwovu hujionesha kuwa jasiri,lakini mwadilifu huhakikisha ametenda sawa.

30. Hakuna hekima, maarifa, wala mawaidha yoyote ya mtu,yawezayo kumshinda Mwenyezi-Mungu.

31. Farasi hutayarishwa kwa vita,lakini ushindi wamtegemea Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Methali 21