Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 20:6-19 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Watu wengi hujivunia kuwa wema,lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?

7. Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu;watoto wake atakaowaacha watabarikiwa.

8. Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu,huupepeta uovu wote kwa macho yake.

9. Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu;mimi nimetakasika dhambi yangu?”

10. Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu,vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

11. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,kama tabia yake ni njema na aminifu.

12. Sikio lisikialo na jicho lionalo,yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.

13. Usipende kulala tu usije ukawa maskini;uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi.

14. “Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika,lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.

15. Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa;lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!

16. Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni,chukua nguo yake;mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.

17. Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu,lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.

18. Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana;ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.

19. Mpiga domo hafichi siri,kwa hiyo mwepe mtu wa kuropoka.

Kusoma sura kamili Methali 20