Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 20:11-28 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,kama tabia yake ni njema na aminifu.

12. Sikio lisikialo na jicho lionalo,yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.

13. Usipende kulala tu usije ukawa maskini;uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi.

14. “Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika,lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.

15. Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa;lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!

16. Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni,chukua nguo yake;mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.

17. Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu,lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.

18. Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana;ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.

19. Mpiga domo hafichi siri,kwa hiyo mwepe mtu wa kuropoka.

20. Anayemlaani baba yake au mama yake,mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani.

21. Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni,haitakuwa ya heri mwishoni.

22. Usiseme, “Nitalipiza ubaya niliotendewa.”Mtegemee Mwenyezi-Mungu naye atakusaidia.

23. Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,na vipimo visivyo halali ni kitu kibaya.

24. Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu;awezaje binadamu kujua njia ya kwenda?

25. Ni hatari kusema kwa mzaha “Usiahidi kumpa Mungu kitu bila kufikiri,la sivyo utaanza kusikitika baada ya nadhiri yako.”

26. Mfalme mwenye busara huwapepeta waovu;huwaadhibu bila huruma.

27. Dhamiri ya mtu ni taa ya Mwenyezi-Mungu;huchunguza nafsi yake mtu mpaka ndani kabisa.

28. Wema na uaminifu humkinga mfalme;utawala wake huimarishwa kwa uadilifu.

Kusoma sura kamili Methali 20