Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 19:22-29 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Kinachotakiwa kwa mtu ni uaminifu;afadhali mtu maskini kuliko mtu mwongo.

23. Kumcha Mwenyezi-Mungu kunaleta uhai;amchaye hujaliwa pumziko la kutosheleza,wala hatapatwa na baa lolote.

24. Mvivu ni kama mtu atiaye mkono katika sahani ya chakula,lakini hana nguvu ya kuuinua hadi mdomoni.

25. Mwadhibu mwenye mzaha naye mjinga atapata akili;mwonye mwenye busara naye atapata maarifa.

26. Anayemdhulumu baba yake na kumfukuza mama yake,ni mtoto asiyefaa na mpotovu.

27. Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,utapotea mara mbali na maneno ya hekima.

28. Shahidi asiyefaa kitu huidhihaki haki;na kinywa cha mwovu hubugia uovu.

29. Adhabu iko tayari kwa wenye mzaha,mijeledi imetayarishwa kuchapa migongo ya wapumbavu.

Kusoma sura kamili Methali 19