Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 18:5-14 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Si vizuri kumpendelea mtu mwovu,na kumnyima haki mtu mwadilifu.

6. Maneno ya mpumbavu huleta ugomvi;kila anachosema husababisha adhabu.

7. Kinywa cha mpumbavu humwangamiza mwenyewe;mdomo wake ni mtego wa kumnasa yeye mwenyewe.

8. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo kitamu;ambacho hushuka moja kwa moja mpaka tumboni.

9. Mtu mvivu kazini mwakeni ndugu yake mharibifu.

10. Jina la Mwenyezi-Mungu ni mnara imara;mwadilifu huukimbilia akawa salama.

11. Lakini tajiri hudhani mali ni ngome yake;anafikiri hayo ni ukuta mrefu unaomlinda.

12. Majivuno ya moyoni huleta maangamizi,lakini unyenyekevu huleta heshima.

13. Kujibu kabla ya kusikilizani upumbavu na jambo la aibu.

14. Roho ya mtu huweza kustahimili ugonjwa,lakini ukiwa umevunjika moyo, utastahimilije?

Kusoma sura kamili Methali 18