8. Mtu husifiwa kadiri ya hekima yake,lakini mtu wa fikira mbaya hudharauliwa.
9. Afadhali mtu wa chini anayejitegemea,kuliko ajitakiaye makuu na kukosa chakula.
10. Mtu mwadilifu huwajali wanyama wake,lakini huruma ya mwovu ni ukatili.
11. Mkulima mwenye bidii ana chakula tele,lakini afuataye mambo yasiyofaa hana akili.
12. Waovu hutamani faida isiyo halali,lakini mtu mwadilifu husimama imara.