Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 12:4-22 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Mke mwema ni taji ya fahari kwa mumewe;amwaibishaye mumewe ni kama kidonda mifupani mwake.

5. Mawazo ya mwadilifu ni ya haki;mashauri ya mwovu ni ya udanganyifu.

6. Maneno ya waovu lengo lake ni kuua,lakini maneno ya waadilifu huwaokoa wanaotishwa.

7. Waovu huangamizwa na kutoweka kabisa,lakini jamaa ya waadilifu hudumishwa.

8. Mtu husifiwa kadiri ya hekima yake,lakini mtu wa fikira mbaya hudharauliwa.

9. Afadhali mtu wa chini anayejitegemea,kuliko ajitakiaye makuu na kukosa chakula.

10. Mtu mwadilifu huwajali wanyama wake,lakini huruma ya mwovu ni ukatili.

11. Mkulima mwenye bidii ana chakula tele,lakini afuataye mambo yasiyofaa hana akili.

12. Waovu hutamani faida isiyo halali,lakini mtu mwadilifu husimama imara.

13. Mtu mwovu hunaswa kwa uongo wake mwenyewe,lakini mwadilifu hutoka katika taabu.

14. Mtu hufanikiwa kutokana na maneno yakekama apatavyo matokeo ya kazi za mikono yake.

15. Mpumbavu huiona njia yake kuwa sawa,lakini mwenye hekima husikiliza shauri.

16. Udhia wa mpumbavu hujulikana mara,lakini mwerevu huyapuuza matukano.

17. Msema kweli hutoa ushahidi wa kweli,lakini shahidi wa uongo hutamka udanganyifu.

18. Maneno ya ovyo hujeruhi kama upanga,lakini asemayo mwenye hekima huponesha kidonda.

19. Ukweli hudumu milele,lakini uongo ni wa kitambo tu.

20. Wanaopanga maovu wamejaa udanganyifu moyoni,lakini wanaonuia mema hupata furaha.

21. Waadilifu hawapatwi na jambo lolote baya,lakini waovu wamejaa dhiki.

22. Midomo isemayo uongo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini watu waaminifu ni furaha yake.

Kusoma sura kamili Methali 12