Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 10:23-32 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;lakini watu wenye busara hufurahia hekima.

24. Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata,lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.

25. Kimbunga hupita na mwovu hutoweka,lakini mwadilifu huimarishwa milele.

26. Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.

27. Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha,lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.

28. Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha,lakini tazamio la mwovu huishia patupu.

29. Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu,lakini watendao maovu atawaangamiza.

30. Waadilifu kamwe hawataondolewa nchini,lakini waovu hawatakaa katika nchi.

31. Kinywa cha mwadilifu hutoa mambo ya hekima,lakini ulimi wa mtu mbaya utakatiliwa mbali.

32. Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika,lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Kusoma sura kamili Methali 10