Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 10:2-19 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai,lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni.

3. Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa,lakini huzipinga tamaa za waovu.

4. Uvivu husababisha umaskini,lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha.

5. Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno,kulala wakati wa kuvuna ni aibu.

6. Mwadilifu hujiletea baraka yeye mwenyewe,lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.

7. Waadilifu hukumbukwa kwa baraka,lakini waovu watasahaulika kabisa.

8. Mwenye hekima moyoni hutii amri,lakini mpumbavu aropokaye ataangamia.

9. Aishiye kwa unyofu huishi salama,apotoshaye maisha yake atagunduliwa.

10. Akonyezaye kwa nia mbaya huzusha taabu,lakini aonyaye kwa ujasiri huleta amani.

11. Kinywa cha mwadilifu ni chemchemi ya uhai,lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.

12. Chuki huzusha ugomvi,lakini upendo hufunika makosa yote.

13. Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima,lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni.

14. Wenye hekima huhifadhi maarifa,lakini kuropoka kwa mpumbavu huleta maangamizi haraka.

15. Mali ya tajiri ndio ngome yake,umaskini wa maskini humletea maangamizi.

16. Tuzo la mtu mwema ni uhai,lakini mwovu huishia katika dhambi.

17. Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai,lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

18. Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki,anayemsingizia mtu ni mpumbavu.

19. Penye maneno mengi hapakosekani makosa,lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.

Kusoma sura kamili Methali 10