Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 10:16-26 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Tuzo la mtu mwema ni uhai,lakini mwovu huishia katika dhambi.

17. Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai,lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

18. Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki,anayemsingizia mtu ni mpumbavu.

19. Penye maneno mengi hapakosekani makosa,lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.

20. Maneno ya mwadilifu ni kama fedha bora;akili ya mtu mwovu haina thamani yoyote.

21. Maneno ya mwadilifu huwafaa watu wengi,lakini wapumbavu hufa kwa kukosa akili.

22. Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka,juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.

23. Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;lakini watu wenye busara hufurahia hekima.

24. Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata,lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.

25. Kimbunga hupita na mwovu hutoweka,lakini mwadilifu huimarishwa milele.

26. Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.

Kusoma sura kamili Methali 10