Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 10:13-29 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima,lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni.

14. Wenye hekima huhifadhi maarifa,lakini kuropoka kwa mpumbavu huleta maangamizi haraka.

15. Mali ya tajiri ndio ngome yake,umaskini wa maskini humletea maangamizi.

16. Tuzo la mtu mwema ni uhai,lakini mwovu huishia katika dhambi.

17. Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai,lakini anayekataa kuonywa amepotoka.

18. Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki,anayemsingizia mtu ni mpumbavu.

19. Penye maneno mengi hapakosekani makosa,lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.

20. Maneno ya mwadilifu ni kama fedha bora;akili ya mtu mwovu haina thamani yoyote.

21. Maneno ya mwadilifu huwafaa watu wengi,lakini wapumbavu hufa kwa kukosa akili.

22. Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka,juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.

23. Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;lakini watu wenye busara hufurahia hekima.

24. Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata,lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.

25. Kimbunga hupita na mwovu hutoweka,lakini mwadilifu huimarishwa milele.

26. Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.

27. Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha,lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.

28. Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha,lakini tazamio la mwovu huishia patupu.

29. Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu,lakini watendao maovu atawaangamiza.

Kusoma sura kamili Methali 10