Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 1:8-19 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako;

9. hayo yatakupamba kilemba kichwani pako,kama mkufu shingoni mwako.

10. Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi.

11. Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua;njoo tukawashambulie wasio na hatia!

12. Tutawameza kama Kuzimu wakiwa hai,watakuwa kama wale washukao Shimoni.

13. Tutajitwalia mali zote za thamani,nyumba zetu tutazijaza nyara.

14. Njoo ushirikiane nasi,vyote tutakavyopata tutagawana.”

15. Wewe mwanangu usiandamane nao,uzuie mguu wako usifuatane nao.

16. Maana wao wako mbioni kutenda maovu,haraka zao zote ni za kumwaga damu.

17. Mtego utegwao huku ndege anaona,mtego huo wategwa bure.

18. Wao huvizia na kujiangamiza wao wenyewe,hutega mtego wa kujinasa wao wenyewe.

19. Ndivyo zilivyo njia za waishio kwa ukatili;ukatili huyaangamiza maisha ya wakatili.

Kusoma sura kamili Methali 1