Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 1:23-33 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Sikilizeni maonyo yangu;nitawamiminia mawazo yangu,nitawajulisha maneno yangu.

24. Kwa kuwa nimewaita mkakataa kusikiliza,nimewapungia mkono mje mkakataa,

25. mkapuuza mashauri yangu yote,wala hamkuyajali maonyo yangu,

26. nami pia nitayachekelea maafa yenu,nitawadhihaki mnapokumbwa na hofu,

27. hofu itakapowakumba kama tufani,maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga,wakati udhia na dhiki vitakapowapata.

28. Hapo ndipo mtakaponiita lakini sitaitika;mtanitafuta kwa bidii lakini hamtanipata.

29. Kwa kuwa mliyachukia maarifa,wala hamkuchagua kumcha Mwenyezi-Mungu;

30. maadamu mlikataa shauri langu,mkayapuuza maonyo yangu yote;

31. basi, mtakula matunda ya mienendo yenu,mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe.

32. Maana wajinga hujiua kwa ukaidi wao,wapumbavu hujiangamiza kwa kujiamini kwao.

33. Lakini kila anisikilizaye atakaa salama,atatulia bila kuogopa mabaya.”

Kusoma sura kamili Methali 1