Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 1:18-28 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Wao huvizia na kujiangamiza wao wenyewe,hutega mtego wa kujinasa wao wenyewe.

19. Ndivyo zilivyo njia za waishio kwa ukatili;ukatili huyaangamiza maisha ya wakatili.

20. Hekima huita kwa sauti barabarani,hupaza sauti yake sokoni;

21. huita juu ya kuta,hutangaza penye malango ya mji:

22. “Enyi wajinga! Mpaka lini mtapenda kuwa wajinga?Mpaka lini wenye dharau watafurahia dharau zao,na wapumbavu kuchukia maarifa?

23. Sikilizeni maonyo yangu;nitawamiminia mawazo yangu,nitawajulisha maneno yangu.

24. Kwa kuwa nimewaita mkakataa kusikiliza,nimewapungia mkono mje mkakataa,

25. mkapuuza mashauri yangu yote,wala hamkuyajali maonyo yangu,

26. nami pia nitayachekelea maafa yenu,nitawadhihaki mnapokumbwa na hofu,

27. hofu itakapowakumba kama tufani,maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga,wakati udhia na dhiki vitakapowapata.

28. Hapo ndipo mtakaponiita lakini sitaitika;mtanitafuta kwa bidii lakini hamtanipata.

Kusoma sura kamili Methali 1