Agano la Kale

Agano Jipya

Methali 1:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi.

2. Methali hizi zawapatia watu hekima na nidhamu; zawafanya waelewe maneno ya busara,

3. zawafanya kuwa na nidhamu, utaratibu, uadilifu, haki na kutenda kwa usawa.

4. Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari.

5. Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo.

6. Mtu aelewe methali na mifano, maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao.

7. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa,lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

8. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako;

9. hayo yatakupamba kilemba kichwani pako,kama mkufu shingoni mwako.

10. Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi.

11. Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua;njoo tukawashambulie wasio na hatia!

12. Tutawameza kama Kuzimu wakiwa hai,watakuwa kama wale washukao Shimoni.

Kusoma sura kamili Methali 1