Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 4:7-15 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji,walikuwa weupe kuliko maziwa.Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe,uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.

8. Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa,wanapita barabarani bila kujulikana;ngozi yao imegandamana na mifupa yaoimekauka, imekuwa kama kuni.

9. Afadhali waliouawa kwa upangakuliko waliokufa kwa njaa,ambao walikufa polepolekwa kukosa chakula.

10. Kina mama ambao huwa na huruma kuuwaliwapika watoto wao wenyewe,wakawafanya kuwa chakula chaowakati watu wangu walipoangamizwa.

11. Mwenyezi-Mungu alionesha uzito wa ghadhabu yake,aliimimina hasira yake kali;aliwasha moto huko mjini Siyoniambao uliteketeza misingi yake.

12. Wafalme duniani hawakuaminiwala wakazi wowote wa ulimwenguni,kwamba mvamizi au aduiangeweza kuingia malango ya Yerusalemu.

13. Hayo yalisababishwa na dhambi za manabii wake,yalitukia kwa sababu ya uovu wa makuhani wakeambao walimwaga damu ya waadilifu mjini kwake.

14. Walitangatanga barabarani kama vipofu,walikuwa wamekuwa najisi kwa damu,hata asiwepo mtu yeyote wa kuwagusa.

15. Watu waliwapigia kelele wakisema:“Tokeni, nendeni zenu enyi mlio najisi!Tokeni, tokeni, msiguse chochote.”Hivyo wakawa wakimbizi na kutangatanga;watu wa mataifa walitamka:“Hawa hawatakaribishwa kukaa kwetu!”

Kusoma sura kamili Maombolezo 4