Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 4:14-22 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Walitangatanga barabarani kama vipofu,walikuwa wamekuwa najisi kwa damu,hata asiwepo mtu yeyote wa kuwagusa.

15. Watu waliwapigia kelele wakisema:“Tokeni, nendeni zenu enyi mlio najisi!Tokeni, tokeni, msiguse chochote.”Hivyo wakawa wakimbizi na kutangatanga;watu wa mataifa walitamka:“Hawa hawatakaribishwa kukaa kwetu!”

16. Mwenyezi-Mungu mwenyewe aliwatawanya,wala hatawajali tena.Makuhani hawatapata tena heshima,wazee hawatapendelewa tena.

17. Tulichoka kukaa macho kungojea msaada;tulikesha na kungojea kwa hamutaifa ambalo halikuweza kutuokoa.

18. Watu walifuatilia hatua zetu,tukashindwa kupita katika barabara zetu.Siku zetu zikawa zimetimia;mwisho wetu ukawa umefika.

19. Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai,walitukimbiza milimani,walituvizia huko nyikani.

20. Walimnasa yule ambaye maisha yetu yalimtegemea,yule mfalme aliyewekwa wakfu wa Mwenyezi-Mungu,yule ambaye tulisema: “Chini ya ulinzi waketutaishi miongoni mwa mataifa.”

21. Wakazi wa Edomu, mwaweza kushangilia kwa sasa,mwaweza kwa sasa kufurahi enyi wakazi wa Uzi;lakini kikombe hiki cha adhabu kitawajia pia,nanyi pia mtakinywa na kulewa,hata mtayavua mavazi yenu!

22. Adhabu ya uovu wako ewe Siyoni imekamilika;Mwenyezi-Mungu hatawaacha zaidi uhamishoni.Lakini nyinyi Waedomu atawaadhibu kwa uovu wenu,atazifichua dhambi zenu.

Kusoma sura kamili Maombolezo 4