Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 4:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Jinsi gani dhahabu yetu ilivyochujuka,dhahabu safi kabisa ilivyobadilika!Mawe ya thamani yametawanywayamesambaa barabarani kote.

2. Watoto wa Siyoni waliosifika sana,waliothaminiwa kama dhahabu safi,jinsi gani sasa wamekuwa kama vyombo vya udongo,kazi ya mikono ya mfinyanzi!

3. Hata mbwamwitu huwa na hisia za mamana kuwanyonyesha watoto wao;lakini watu wangu wamekuwa wakatili,hufanya kama mbuni nyikani.

4. Midomo ya watoto wachanga imekauka kwa kiu,watoto wanaomba chakula lakini hakuna anayewapa.

5. Watu waliojilisha vyakula vinonosasa wanakufa njaa barabarani.Waliolelewa na kuvikwa kifalmesasa wanafukua kwa mikono kwenye majaa.

6. Watu wangu wamepata adhabu kubwakuliko watu wa mji wa Sodomamji ambao uliteketezwa ghaflabila kuwa na muda wa kunyosha mkono.

7. Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji,walikuwa weupe kuliko maziwa.Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe,uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.

8. Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa,wanapita barabarani bila kujulikana;ngozi yao imegandamana na mifupa yaoimekauka, imekuwa kama kuni.

9. Afadhali waliouawa kwa upangakuliko waliokufa kwa njaa,ambao walikufa polepolekwa kukosa chakula.

10. Kina mama ambao huwa na huruma kuuwaliwapika watoto wao wenyewe,wakawafanya kuwa chakula chaowakati watu wangu walipoangamizwa.

11. Mwenyezi-Mungu alionesha uzito wa ghadhabu yake,aliimimina hasira yake kali;aliwasha moto huko mjini Siyoniambao uliteketeza misingi yake.

Kusoma sura kamili Maombolezo 4